Diamond azungumzia ujumbe alioandika Wema Sepetu kuhusu tatizo lake la kutopata mtoto!

wpid-wema-akiwa-pembeni-kumsupport-diamond1.jpg       Kwa muda mrefu, Diamond Platnumz alikuwa akilijua tatizo la mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu la kutoshika mimba.Akiongea na kipindi cha Ng’ari Ng’ari cha Clouds TV, Diamond alisema wakati wako pamoja waliwahi kuzunguka kwa wataalam mbalimbali kujaribu kupata tiba lakini hawakufanikiwa.
Alisema ilifika wakati alimweleza tu kuwa akubali hali hiyo.
Kuhusu kile Wema alichokiandika kwenye Instagram hivi karibuni ambapo alieleza ukweli wa hali yake ya kutopata mtoto, Diamond alisema ujumbe huo ulimuumiza kama wengine walivyoumia.
Alisema alikuwa anafahamu jinsi watu wanavyomshambulia Wema kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kutopata mtoto na amemsifia kwa kuusema ukweli.
Hata hivyo aliwashauri watumiaji wa mtandao ya kijamii kuitumia vyema na sio kuitumia kuwatusi mastaa wao kwakuwa ni kweli maneno yao huwaumiza kama binadamu wengine.

Post a Comment

0 Comments