JOHARI AMBWAGA RAY HADHARANI!!,AKANA KUWAHI KUWA NA MAHUSIANO NAYE!!


Staa wa Bongo Movies na mmiliki mwenza wa kampuni ya filamu nchini ya ‘RJ Company’, Blandina Chagula ‘Johari’, ameibuka na kushangaza wengi kwa kauli yake kwamba hakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji mwenzake, Vicent Kigosi ‘Ray’.
Staa huyo aliwahi kukiri kuwa na uhusiano huo na msanii huyo na kwamba walishaachana kwa amani, ndiyo maana waliweza kuendelea na kampuni yao ya masuala ya filamu ya Rj Company.


Juzi Johari ameliambia gazeti la Mtanzania kwamba, muda mrefu alikuwa akisikiliza wanaodai hana uelewano mzuri na Ray kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji Chuchu Hans na sasa ameamua kuweka wazi suala hilo.
“Ni kwa kipindi kirefu sana yamezuka maneno yanayodai mimi na Ray tulishawahi kuwa wapenzi, kitu ambacho si cha kweli, tena kibaya zaidi wameongeza kuwa hatuna maelewano mazuri kikazi,” alieleza Johari.
Aliendelea kufafanua: “Sikuwahi kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi kama wengi wanavyofikiria na kama ningekuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ray na tumeachana, hata kampuni yetu ingeshavunjika kwa kuwa tungekuwa na chuki, nawaambia hatutegemei kutengana kikazi wala kirafiki,” alisema Johari 

Post a Comment

0 Comments