Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, JUMA NKAMIA WATCH THESE VIDEOS

Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, JUMA NKAMIA WATCH THESE VIDEOS Waandishi watakiwa kufuata maadili kampeni ya uchunguzi wa Saratani ya matiti Oparesheni ya kukamata mazao ya misitu Noti bandia mkoani Tanga Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, JUMA NKAMIA, amewataka waandishi wa habari nchini kufuata maadili ya taaluma hiyo ili kuzuia vyombo vyao vya habari visipate adhabu ya kufungiwa kwakukiuka maadili ikiwa ni pamoja na kuonyesha picha zisizofaa katika jamii. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo ya Radio TRIPPLE A ya jijini ARUSHA, amesema hivi sasa serikali haitavumilia chombo chochote cha habari pamoja na wananchi wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kwakuweka picha za watu waliopoteza maisha au waliopata ajali kwani kwakufanya hivyo ni kukiuka maadhili. Pia amesema vyombo vingi vya habari vimejisahau na sasa vinaangalia soko ambalo linasababisha ukiukwaji mkubwa wa maadili ya uendeshwaji wa vyombo hivyo ambayo yapo kisheria na vyombo hivyo vinayafahamu. Kufuatia kauli hiyo lakini pia amesema,hivi sasa vyombo vingi vimesahau malengo makuu yakuanzishwa ikiwa ni pamoja na kuelimisha, kuburudisha pamoja na kuhabarisha kwani hivi vyombo vingi vinaburudisha tu kwakupiga muziki. Mkurugenzi wa TRIPPLE A Radio,PAPAKING MOLELI, amesema watahakikisha wanafuata maadili ya taaluma ya habari nchini. Naye Meneja wa Mamlaka ya mawasiliano nchini Kanda ya Kaskazini, ameonya mitandao ya kijamii isitumike vibaya kwakuweka picha zenye kudhalilisha kwani ni ukiukwaji wakuanzishwa kwa mitandao hiyo. Aidha amesema hakuna sababu yakukaa kimya pasipokufuatilia watu wanaotumia mitandao hiyo ya kijamii vibaya.

Post a Comment

0 Comments