Watu 4 washikiliwa na polisi mkoani MANYARA

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa MANYARA Kamishna Msaidizi wa Polisi CHRISTOPHER FUIME
Jeshi la Polisi Mkoani MANYARA linawashikilia vijana WANNE kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la unyang'anyi wa kutumia nguvu, na kupora mali za raia mmoja wa kigeni kutoka VIETNAM, TRUONG BIOVU katika eneo la makutano ya barabara kuu iendayo ARUSHA na MALANGII.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa MANYARA Kamishna Msaidizi wa Polisi CHRISTOPHER FUIME amesema kuwa vijana hao walikuwa ni waajiriwa wa raia huyo wa kigeni wakifanyakazi ya kutandaza nyaya za mkongo wa Taifa kutoka BABATI kwenda ARUSHA kupitia Kampuni ya VIATEL.

Kamishna Msaidizi FUIME ameiambia TBC kuwa vijana hao WANNE wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 na 30, wanatuhumiwa kumpora mwajiri wao mfuko uliokuwa na fedha pamoja na simu na kuwataja kuwa ni KILIAN PETER, SHAFII MOHAMED, JOHANES SAID na MOHAMED SHAABAN, wote wakazi wa Mjini BABATI.

Kamanda FUIME amewataka raia wa kigeni wanaofanyakazi Mkoani MANYARA kuchukua tahadhari wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Post a Comment

0 Comments